Mtandao wa Wanawake Watetezi wa Haki za Binadamu tumefanya kikao na watumishi wa Serikali wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Idara ya Maendeleo ya jamii kuona namna ya kuimarisha mifumo ya kuwezesha mazingira salama ya Wanawake Watetezi wa Haki za Binadamu hapa nchini. Kikao hiki ni moja ya kuweka mahusiano kati ya Wizara pamoja na Mtandao wa Wanawake watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania. Vile vile, Mtandao ulitumia wasaa huu kutambulisha kazi na shughuli zinazofanywa na Mtandao wa Wanawake watetezi pamoja na kutambulisha mradi wetu wenye lengo la kuwezesha wanawake watetezi kuelewa mifumo ya Ulizi na usalama ambayo inaweza kuwa ni moja ya fursa kwa wanawake watetezi kufanya shughuli zao kwenye mazingira salama. Mwanamke Mtetezi mstahamilivu kwa mabadiliko ya jamii ni nguzo muhimu katika kuendeleza na kulinda haki za Binadamu hapa nchini. Wanawake Watetezi wa Haki za Binadamu wanabeba jukumu kubwa katika Jamii kwa ajili ya mabadiliko. Kikao kiliweza kushauri mambo mengi ikiwemo utendaji wa kazi wa watumishi wa serikali namna ya kutumia mifumo iliopo katika kuhakikisha kuna mazingira wezeshi na salama kwa Wanawake Watetezi. Kikao hiki kilihudhuriwa na Bi. Juliana Kibonde Kaimu Mkurugenzi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii na Jinsia na Bw.Josiah P.Saoke ambaye Afisa wa Idara ya Maendeleo,jinsia na Wanawake na Kutoka mtandao huu, Mratibu wa Taifa Bi. Hilda S. Dadu pamoja na Bi Suzana Charles Afisa Ulinzi na Sheria.

IMETOLEWA NA MTANDAO WA WANAWAKE WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU TANZANIA 9 Aprili, 2024

Members

78

Members Registered

Litigation

2

Cases Intervened

Projects

5

Projects Completed

Copyright © CWHRDs-Tanzania